Makala: Faida ya Maziwa ya Mbuzi kwa Wagonjwa wa Kisukari

0

Ingawa maziwa ya mbuzi si tiba ya ugonjwa wa kisukari, wataalamu wanasisitiza kuwa yanaweza kuwa nyongeza muhimu katika lishe ya wagonjwa

Muhtasari wa Makala: Faida ya Maziwa ya Mbuzi kwa Wagonjwa wa Kisukari

Makala haya yanaangazia umuhimu wa maziwa ya mbuzi kama sehemu ya lishe bora kwa wagonjwa wa kisukari. Yanaeleza historia ya matumizi ya maziwa ya mbuzi duniani na nchini Kenya, ambapo ufugaji wa mbuzi umeenea hasa katika maeneo ya ukame  kama Turkana, Marsabit, Garissa, Wajir, Samburu na Baringo.

Kupitia maoni ya wataalamu wa afya, wakulima na watumiaji wa maziwa ya mbuzi, makala yanaeleza kuwa maziwa haya yana virutubisho muhimu kama protini, vitamini na madini yanayoweza kusaidia kuboresha afya kwa ujumla. Aidha, yanaelezwa kuwa rahisi kumeng’enywa na yanaweza kusaidia mwili kudhibiti kiwango cha sukari kwenye damu yanapotumiwa kama sehemu ya lishe bora.

Ingawa maziwa ya mbuzi si tiba ya ugonjwa wa kisukari, wataalamu wanasisitiza kuwa yanaweza kuwa nyongeza muhimu katika lishe ya wagonjwa pamoja na mazoezi, ushauri wa kitabibu na matumizi sahihi ya dawa. Makala pia yanaonyesha jinsi ongezeko la mahitaji ya maziwa ya mbuzi linavyochangia ukuaji wa sekta ya ufugaji nchini Kenya.

Makala haya yameandaliwa na kuripotiwa na Emmanuel Kipkoech, mwanafunzi wa taaluma ya uandishi wa habari kutoka ICS Technical College, anayefanya mafunzo ya kitaaluma  Eldoret Media Hub.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *