Gavana Bii Aongoza Sherehe za Jamhuri, Turbo

0

“Ningependa kuwaambia wale wanyakuzi wa ardhi ya umma wairudishe mara moja kabla ya kutafutwa na maafisa wa EACC” alisema gavana.

Sherehe za Jamhuri zaadhimishwa katika eneo bunge la Turbo.

Na Wesley Kiplimo

Sherehe za maadhimisho ya Sikukuu ya Jamhuri katika Kaunti ya Uasin Gishu zimefanyika katika shule ya msingi ya Cheramei Jua kali eneo bunge la Turbo.

Akizungumza katika hafla hiyo, gavana wa kaunti hiyo, Jonathan Bii Chelilim, ambaye alikuwa mgeni wa heshima, amewapongeza wananchi wote waliojitokeza uwanjani.

Alisema kuwa jamhuri ni siku muhimu ya kukumbuka wote waliojitolea kuletea taifa hili uhuru.

Gavana pia ametumia nafasi hiyo kuwaonya vikali wale wote ambao wemenyakua ardhi ya umma kurudisha haraka iwezekanavyo.

“Ningependa kuwaambia wale wanyakuzi wa ardhi ya umma wairudishe mara moja kabla ya kutafutwa na maafisa wa EACC” alisema gavana.

“Wengine hata hunyakua ardhi hata zilizo kwenye vituo vya polisi” aliongezea Bii.

Vilevile,Maria Busolo, kutoka eneo la Turbo ameitaka serikali ya Gavana Bii kuwakumbuka kina mama katika shughuli za maendeleo.

“Tunaomba tufunguliwe biashara na kufadhiliwa katika ukulima hasa wa parachichi na ufugaji wa kuku” amesema Busolo.

Kamishna wa Kaunti ya Uasin Gishu Eddyson Nyale ,aliyesoma hotuba ya Rais William Rutto, amewarai wananchi wa kaunti hiyo kuwa na umoja na ushirikiano huku wakifuata nyayo za wazee wetu waliopigania uhuru tunaojivunia hii leo.

Huku akiwaonya wezi wa mifugo ambao wameonekana kuwa kero kwa wananchi wa eneo la Turbo.

Maadhimisho na shamrashamra hizo zimefanyika kwa mara ya kwanza katika eneo bunge la Turbo. Mbunge wa eneo hilo Janet Sitienei hakuwepo katika sherehe hizo.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *