Makala ya Redio: “Virusi vya Jahanamu”

0

Katika jiji la Eldoret, mvulana anayeitwa John (jina lake halisi limefichwa) anakumbuka alipougua kaswende alipomaliza shule ya upili

An image depicting-the-impact-of-sexually-transmitted-diseases-STDs-among-young-africans/Hubz Ai

 

 

Muhtasari wa Kipindi cha Redio “Virusi vya Jahanamu”

Kulingana na ripoti ya Shirika la Afya Duniani (WHO), zaidi ya watu milioni moja huambukizwa magonjwa ya zinaa kila siku, huku idadi ya maambukizi ikiongezeka hasa miongoni mwa vijana. Magonjwa haya ni pamoja na kisonono, kaswende, Ukimwi, na clamidia, ambayo mara nyingi huonekana kwa dalili kama maumivu wakati wa haja ndogo, vipele sehemu za siri, na maumivu ya tumbo kwa wanawake.

Katika jiji la Eldoret, mvulana anayeitwa John (jina lake halisi limefichwa) anakumbuka alipougua kaswende alipomaliza shule ya upili. Mtaalamu wa afya, Janet Atieno, anaeleza kuwa maambukizi haya yanachangiwa na ngono zembe, hasa miongoni mwa vijana wenye umri wa miaka 15-24. Changamoto nyingine ni wanafunzi wanaoingia katika mahusiano na watu wazee, maarufu kama “sponsor,” na matumizi ya dawa za kulevya yanayochangia tabia hatarishi.

Pia, umaskini unachangia maambukizi haya kutokana na ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi na vifaa vya kinga, huku vijana wengi wakikosa kondomu za bure. Ili kujikinga, vijana wanashauriwa kujiepusha na ngono zembe na kutumia kinga.

Nikiripoti kutoka Kaunti ya Uasin Gishu, jina langu ni Makena Kimathi.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *