Mikakati yabuniwa kukipa umaarufu chama cha UDA kaunti ya Mombasa na Ukanda wa Pwani

0

Wanachama wa chama cha UDA Mombasa/photo Agnes Mtengo

By Agnes Mtengo 

 

Vuguvugu la hustler Nation chini ya chama Cha UDA kaunti  Mombasa limebuni Mikakati ya  kukipa nguvu chama hicho kukita mizizi Mombasa na Pwani kwa ujumla.

 

Vuguvugu hilo  likiongozwa na  Mshirikishi wa chama hicho kaunti hiyo Samir Omar  limeeleza kuwa mikakati hiyo inalenga kuendeleza mipango ya kusajili wanachama zaidi Katika harakati za kuimarisha udhabiti wa chama cha UDA chini ya mungano wa chama  kinachotawala cha Kenya Kwanza ili  kufanikisha agenda na malengo ya Rais William Ruto ya kuwaunganisha  wakenya.

 

Akizungumza Katika hafla ya kumpokea kiongozi wa  wakfu wa KITAKA FOUNDATION, ndani ya chama hicho Omar, ameeleza matumaini ya kuongeza umaarufu wa Chama Cha UDA eneo la  pwani.

 

 

VuguVugu labuniwa Kukipa Umaarufu Chama cha UDA kaunti ya Mombasa na Ukanda wa Pwani /Agnes Mtengo

 

“ Tutazidi kukipigia debe Chama cha UDA eneo la pwani ili kuhakikisha wapwani wote wako ndani ya UDA,Chama  kinachotawala”Alisema Omar

 

Kwa upande wake kiongozi wa wakfu huo Ali  Hamisi  amepongeza hatua ya kupokelewa ndani ya chama na kuahidi kuunga mkono juhudi zote chamani humo kuhakikisha wanaongeza asilimia 40 ya kura zilizopigiwa chama hicho Kaunti ya Mombasa  katika uchaguzi wa Agosti Tisa  hadi kufikia zaidi  ya asilimia 90 katika uchaguzi mkuu  ujao mwaka wa 2027

 

“Tutahakikisha Chama hichi kinapata ungwaji mkono wa hadi asilimia tisini ya watu wetu wa Mombasa na kaunti za ukanda wa pwani kwa jumla kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027,Kama wapwani hatungependelea kuwa nje ya serikali”Alisema  Hamisi

Wakati uo huo aliyawania kiti Cha ubunge eneo la Likoni Kupitia Tiketi ya chama cha UDA Mohammed mwalimu Mwahima ,amesema hatua hiyo pia ni mojawapo ya harakati za kujiandaa na Shughuli za  uchaguzi katika nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho,uchaguzi unaoratibiwa kufanyika mapema mwezi wa pili mwaka ujao.

 

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *