Watu 4,100 hupoteza maisha yao kila siku nchini Kenya kutokana na TB

0

TB Alliance_Nick Herbert photo

By Dianah Chelagat

Ugonjwa wa kifua kikuu unasalia kuwa mojawapo  ya magonjwa  hatari  zaidi ambukizi ulimwenguni.

Kwa mujibu wa  shirila  la Afya Ulimwenguni (WHO )Kila  siku nchini kenya  zaidi ya watu 4,100 hupoteza maisha kutokana  na TB  wengine 28,000 wakiripotiwa  kuugua ugonjwa huu  unaozuilika  na hata kuweza kutibika.

Jitihadi za kimataifa  za kupambana  na TB  zimeokoa  maisha  ya watu million sitini na sita kote ulimwenguni  tangu mwaka wa 2000.

Hata hivyo janga la Covid-19  limerudisha nyuma  juhudi za miaka mingi zilizoafikiwa kutokomesha TB.

Kila mwaka dunia inadhimisha  siku ya kifua kikuu duniani (TB)  Machi 24, lengo likiwa kuhamasisha  umma kuhusu athari za TB kwa  afya ,maswala ya kijamii, na hata  kiuchumi,na pia kushinikiza  juhudi  za kukomesha janga la TB duniani.

Madhimisho ya mwaka huu, yenye kauli mbiu ‘NDIYO! TUNAWEZA KUKOMESHA TB’, yataandaliwa mjini Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu na kutarajiwa kuhuduriwa na rais Dr William Ruto balozi wa marekani humu nchini kati ya  viongozi wengine wa ngazi za juu.

Courtesy

TB imeorodheshwa  kuwa chanzo kikuu cha vifo humu duniani  na imeshikilia nafasi ya nne ya magonjwa yaayosababisha  vifo vingi  duniani.

Inarepotiwa kuwa watu 13,000 Nchini Kenya  wameambukizwa ugonjwa wa TB  miongoni mwao wakiwa watoto 1,600.

Mwaka wa 2021 wakenya 7,785 walirepotiwa kuambukizwa ugonjwa wa TB  idadi hiyo ikiongezeka hadi wakenya 90,841 mwaka wa 2022.

Zaidi ya asilimia hamsini ya walioambukizwa TB walikuwa kati ya umri wa  miaka25-54.

Kote Ulimwenguni Mwaka wa 2021  idadi ya wanaume waliogonjeka Tb ilikuwa million sita wanawake wakiwa million tatu nukta nne na idadi ya watoto  ikiwa million moja nukta mbili.

Kifua kikuu (TB) husababishwa na aina ya bakteria inayofahamika kama Mycobacterium tuberculosis. Huenezwa wakati mtu aliye na ugonjwa wa TB katika mapafu yake anapokohoa au kupiga chafya na mtu mwingine anavuta matone hayo, ambayo yana bakteria ya TB.

Courtesy

Dalili za kawaida  za maambukizi  ya kifua kikuu  kinacholeta  madhara ni kikohozi sugu na kukohoa damu, kohozi, homa , kutokwa na jasho usiku na hata mtu kupunguka uzani wa mwili.Shirikala USAID siku ya Ijumaa lilitangaza kuwa dola milioni 57 zitatolewa kwa juhudi zinazohitajika za haraka za kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) katika nchi saba zenye mzigo mkubwa wa ugonjwa huu na ambazo ni pamoja na – Afrika Kusini, Bangladesh, India, Indonesia, Ufilipino, Tajikistan na Ukraine.

Mwaka jana katika siku ya kuadhimisha siku ya kifua kikuu,  aliyekuwa waziri wa afya  daktari Mutahi Kagwe ilielezea kwamba serikali ilitarajia  kutoa asilimia  thelathini  na nane  nukta tano za dawa ya kifua kikuu  kwa wakenya kufikia  mwaka 2024 baada ya kuchukua jukumu la kununua  tiba hizo kutoka kwa wafadhili.

 

 

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *