Watu 4,100 hupoteza maisha yao kila siku nchini Kenya kutokana na TB
TB Alliance_Nick Herbert photo
By Dianah Chelagat
Ugonjwa wa kifua kikuu unasalia kuwa mojawapo ya magonjwa hatari zaidi ambukizi ulimwenguni.
Kwa mujibu wa shirila la Afya Ulimwenguni (WHO )Kila siku nchini kenya zaidi ya watu 4,100 hupoteza maisha kutokana na TB wengine 28,000 wakiripotiwa kuugua ugonjwa huu unaozuilika na hata kuweza kutibika.
Jitihadi za kimataifa za kupambana na TB zimeokoa maisha ya watu million sitini na sita kote ulimwenguni tangu mwaka wa 2000.
Hata hivyo janga la Covid-19 limerudisha nyuma juhudi za miaka mingi zilizoafikiwa kutokomesha TB.
Kila mwaka dunia inadhimisha siku ya kifua kikuu duniani (TB) Machi 24, lengo likiwa kuhamasisha umma kuhusu athari za TB kwa afya ,maswala ya kijamii, na hata kiuchumi,na pia kushinikiza juhudi za kukomesha janga la TB duniani.
Madhimisho ya mwaka huu, yenye kauli mbiu ‘NDIYO! TUNAWEZA KUKOMESHA TB’, yataandaliwa mjini Eldoret katika kaunti ya Uasin Gishu na kutarajiwa kuhuduriwa na rais Dr William Ruto balozi wa marekani humu nchini kati ya viongozi wengine wa ngazi za juu.

TB imeorodheshwa kuwa chanzo kikuu cha vifo humu duniani na imeshikilia nafasi ya nne ya magonjwa yaayosababisha vifo vingi duniani.
Inarepotiwa kuwa watu 13,000 Nchini Kenya wameambukizwa ugonjwa wa TB miongoni mwao wakiwa watoto 1,600.
Mwaka wa 2021 wakenya 7,785 walirepotiwa kuambukizwa ugonjwa wa TB idadi hiyo ikiongezeka hadi wakenya 90,841 mwaka wa 2022.
Zaidi ya asilimia hamsini ya walioambukizwa TB walikuwa kati ya umri wa miaka25-54.
Kote Ulimwenguni Mwaka wa 2021 idadi ya wanaume waliogonjeka Tb ilikuwa million sita wanawake wakiwa million tatu nukta nne na idadi ya watoto ikiwa million moja nukta mbili.
Kifua kikuu (TB) husababishwa na aina ya bakteria inayofahamika kama Mycobacterium tuberculosis. Huenezwa wakati mtu aliye na ugonjwa wa TB katika mapafu yake anapokohoa au kupiga chafya na mtu mwingine anavuta matone hayo, ambayo yana bakteria ya TB.

Courtesy
Dalili za kawaida za maambukizi ya kifua kikuu kinacholeta madhara ni kikohozi sugu na kukohoa damu, kohozi, homa , kutokwa na jasho usiku na hata mtu kupunguka uzani wa mwili.Shirikala USAID siku ya Ijumaa lilitangaza kuwa dola milioni 57 zitatolewa kwa juhudi zinazohitajika za haraka za kukabiliana na ugonjwa wa kifua kikuu (TB) katika nchi saba zenye mzigo mkubwa wa ugonjwa huu na ambazo ni pamoja na – Afrika Kusini, Bangladesh, India, Indonesia, Ufilipino, Tajikistan na Ukraine.
Mwaka jana katika siku ya kuadhimisha siku ya kifua kikuu, aliyekuwa waziri wa afya daktari Mutahi Kagwe ilielezea kwamba serikali ilitarajia kutoa asilimia thelathini na nane nukta tano za dawa ya kifua kikuu kwa wakenya kufikia mwaka 2024 baada ya kuchukua jukumu la kununua tiba hizo kutoka kwa wafadhili.
