Kiatu Kimoja kwa Wakati Mmoja: Safari ya John ya Miaka 40 katika Ufundi wa Viatu
Licha ya changamoto hizo, John anaendelea kufanya kazi na amejitolea katika taaluma yake, ambayo imekuwa ikimsaidia yeye na familia yake kwa miaka mingi.
John ni fundi wa viatu katika mji wa Eldoret ambaye amekuwa akiendesha biashara yake tangu mwaka 1987. Kwa takribani miongo minne, amekuwa akitegemea kazi yake kama chanzo chake kikuu cha mapato na riziki. Licha ya changamoto anazokabiliana nazo, hasa kipato kidogo na ukosefu wa mtaji wa kutosha, John anaridhika na kiasi kidogo anachopata. Biashara yake humwezesha kupata chakula na kukidhi mahitaji mengine ya msingi ya kila siku kwa ajili yake na familia yake.
“Niko na changamoto, kwa sasa kazi yetu iko chini manake tunatafuta fedha klila siku. Kuna wakati biashara iko chini na pia kuna wakati biashara inafanya vizuri. Kile kidogo napata, naridhika nacho.”
Kwa John, kupata wateja na kufanya mauzo ni chanzo kikubwa cha furaha, shangwe na kuridhika. Kila anapofanya mauzo, hupata motisha ya kuendelea kufanya kazi na kuihudumia familia yake. Hata hivyo, anasema kuwa serikali kuu haijafanya mengi kusaidia biashara yake. Pamoja na hayo, anatambua mchango wa serikali ya kaunti, ambayo imemsaidia kupata kibanda/stendi ambapo anaendeshea biashara yake.
“Mimi kwa upande wa serikali, hakuna chochote ambacho imenisaidia, ni bidii yangu tu kwa hii kazi. Chenye napata kidogo kile ndicho kinanisaidia. Pegine tu kwa upande wa serikali waliweza kunisaidia nipate kibanda cha kufanyia kazi, nashukuru.
Licha ya changamoto hizo, John anaendelea kufanya kazi na amejitolea katika taaluma yake, ambayo imekuwa ikimsaidia yeye na familia yake kwa miaka mingi.
