CIPK Kanda ya North Rift Yapongeza Rais Ruto kwa Kusikiliza Kilio cha Wakulima, Yaitaka Serikali Kuharakisha Msaada

0

“Tunampongeza Rais William Ruto kwa kusikia kilio cha wakulima na kutangaza mpango wa kuwasaidia walioathiriwa na ukame. Siku chache zilizopita tulitoa wito kwa serikali kuingilia kati, na tunafarijika kuona kwamba Rais amesikia na kuchukua hatua. Huu ni mfano wa uongozi unaosikiliza wananchi,” alisema Sheikh Bini.

Mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na Wahubiri Kenya (CIPK) Kanda ya North Rift, Sheikh Abubakar Ahmed Bini, akizungumza na wanahabari mjini Eldoret, ambapo alimpongeza Rais William Ruto kwa kutangaza msaada kwa wakulima walioathiriwa na ukame na kuitaka serikali kuharakisha utekelezaji wa mpango huo.

 Mwenyekiti wa Baraza la Maimamu na Wahubiri wa  dini ya Kiislamu (CIPK) Kanda ya North Rift, Sheikh Abubakar Ahmed Bini, amempongeza Rais William Ruto kwa kutangaza mpango wa kuwasaidia wakulima walioathiriwa na ukame wa muda mrefu, akisema hatua hiyo imekuja siku chache baada ya  viongoxzi hao pamoja na wakulima  kutoa tamko likiitaka serikali kuingilia kati kuwaokoa wakulima.

Akizungumza mjini Eldoret, Sheikh Bini alisema hotuba ya Rais Ruto aliyotoa Jumapili mjini Eldoret inaonesha kuwa serikali imesikiliza kilio cha wakulima pamoja na viongozi wa dini waliokuwa wameomba hatua za haraka kuchukuliwa ili kuhakikisha kuna  usalama wa  chakula.

Alikumbusha kuwa siku chache zilizopita, CIPK Kanda ya North Rift ilitoa tamko rasmi ikiitaka serikali  na haswa kw a rasi Ruto kuwasaidia wakulima waliopata hasara kubwa kutokana na ukame ulioathiri mashmaba mengi msimu huu.

“Tunampongeza Rais William Ruto kwa kusikia kilio cha wakulima na kutangaza mpango wa kuwasaidia walioathiriwa na ukame. Siku chache zilizopita tulitoa wito kwa serikali kuingilia kati, na tunafarijika kuona kwamba Rais amesikia na kuchukua hatua. Huu ni mfano wa uongozi unaosikiliza wananchi,” alisema Sheikh Bini.

Kiongozi huyo wa Kiislamu alimshukuru Mwenyezi Mungu kwa mvua zilizonyesha hivi karibuni na kurejesha matumaini kwa wakulima wengi katika eneo la North Rift baada ya miezi kadhaa ya ukame uliosababisha hasara kubwa na kuhatarisha usalama wa chakula.

Aidha, alipongeza ahadi ya Rais ya kuwapatia wakulima pembejeo za kilimo, lakini akaitaka serikali kuharakisha utekelezaji wa mpango huo.

“Tangazo la Rais linatia moyo, lakini kilicho muhimu sasa ni utekelezaji wa haraka. Wakulima wengi walikopa fedha ili kufadhili shughuli zao za kilimo. Kila siku inayopita bila msaada inaongeza mateso yao na kuwaingiza zaidi kwenye madeni,” alisema.

Sheikh Bini alisema wakulima wengi wanakabiliwa na changamoto kubwa za kurejesha mikopo waliyochukua kwa ajili ya maandalizi ya mashamba, mbegu, mbolea na pembejeo nyingine.

“Baadhi ya wakulima wamekata tamaa kutokana na hasara kubwa na madeni yanayoongezeka. Serikali ikitoa msaada kwa wakati, itawarejeshea matumaini, kulinda maisha yao na kuwawezesha kuendelea kuzalisha chakula kwa taifa,” aliongeza.

Kuhusu mjadala wa ruwaza ya mwaka  2060, Sheikh Bini alisema mpango huo unatoa nafasi muhimu ya kuimarisha utawala bora, uwajibikaji na umoja wa kitaifa.

Alihimiza serikali kuhakikisha utekelezaji wa ruwaza hiyo unazingatia kwa dhati Sura ya Sita ya Katiba kuhusu Uongozi na Uadilifu.

“Hakutakuwa na maendeleo ya kweli bila viongozi waadilifu. Vision 2060 inapaswa kujengwa juu ya misingi ya uadilifu, uwajibikaji na matumizi bora ya rasilimali za umma. Sura ya Sita ya Katiba lazima iwe msingi wa maendeleo ya taifa,” alisema.

Pia alitoa wito kwa serikali kuwashirikisha viongozi wa dini katika mijadala ya Vision 2060, akisema wana mchango mkubwa katika kuimarisha maadili, amani, mshikamano wa kitaifa na uwajibikaji.

“Viongozi wa dini wakishirikishwa kikamilifu, watahakikisha kwamba maswala ya maadili yanabakia  kuwa msingi wa maendeleo ya taifa huku wakisaidia kuimarisha uadilifu na kupambana na ufisadi,” alisema.

Kuhusu masuala ya utawala na uwajibikaji, Sheikh Bini alipokea vyema hatua ya Mbunge wa Mukurweini John Kaguchia kuhojiwa na Maafisa wa Idara ya Upelelezi wa Jinai (DCI), akisema sheria inapaswa kutumika kwa usawa bila kujali mirengo ya kisiasa.

“Tunaunga mkono uchunguzi huru na wa haki. Hakuna kiongozi anayepaswa kuwa juu ya sheria. Awe serikalini au upinzani, yeyote atakayebainika kukiuka sheria anapaswa kuwajibishwa kwa mujibu wa Katiba,” alisema.

Aliwataka maafisa wa uchunguzi kutekeleza wajibu wao kwa weledi, haki na bila upendeleo.

Sheikh Bini alihitimisha kwa kuwataka Wakenya kuendelea kudumisha umoja, kuiombea nchi amani na kuwaunga mkono viongozi wanaotanguliza uadilifu, uwajibikaji na maendeleo endelevu ya taifa.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *