Mikakati yabuniwa kukipa umaarufu chama cha UDA kaunti ya Mombasa na Ukanda wa Pwani
Wanachama wa chama cha UDA Mombasa/photo Agnes Mtengo
By Agnes Mtengo
Vuguvugu la hustler Nation chini ya chama Cha UDA kaunti Mombasa limebuni Mikakati ya kukipa nguvu chama hicho kukita mizizi Mombasa na Pwani kwa ujumla.
Vuguvugu hilo likiongozwa na Mshirikishi wa chama hicho kaunti hiyo Samir Omar limeeleza kuwa mikakati hiyo inalenga kuendeleza mipango ya kusajili wanachama zaidi Katika harakati za kuimarisha udhabiti wa chama cha UDA chini ya mungano wa chama kinachotawala cha Kenya Kwanza ili kufanikisha agenda na malengo ya Rais William Ruto ya kuwaunganisha wakenya.
Akizungumza Katika hafla ya kumpokea kiongozi wa wakfu wa KITAKA FOUNDATION, ndani ya chama hicho Omar, ameeleza matumaini ya kuongeza umaarufu wa Chama Cha UDA eneo la pwani.

“ Tutazidi kukipigia debe Chama cha UDA eneo la pwani ili kuhakikisha wapwani wote wako ndani ya UDA,Chama kinachotawala”Alisema Omar
Kwa upande wake kiongozi wa wakfu huo Ali Hamisi amepongeza hatua ya kupokelewa ndani ya chama na kuahidi kuunga mkono juhudi zote chamani humo kuhakikisha wanaongeza asilimia 40 ya kura zilizopigiwa chama hicho Kaunti ya Mombasa katika uchaguzi wa Agosti Tisa hadi kufikia zaidi ya asilimia 90 katika uchaguzi mkuu ujao mwaka wa 2027
“Tutahakikisha Chama hichi kinapata ungwaji mkono wa hadi asilimia tisini ya watu wetu wa Mombasa na kaunti za ukanda wa pwani kwa jumla kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2027,Kama wapwani hatungependelea kuwa nje ya serikali”Alisema Hamisi
Wakati uo huo aliyawania kiti Cha ubunge eneo la Likoni Kupitia Tiketi ya chama cha UDA Mohammed mwalimu Mwahima ,amesema hatua hiyo pia ni mojawapo ya harakati za kujiandaa na Shughuli za uchaguzi katika nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho,uchaguzi unaoratibiwa kufanyika mapema mwezi wa pili mwaka ujao.
