Viongozi wa Kiislamu Washinikiza kuwepo mahakama ya rufaa ya Kadhi Nchini.

0

Mahakama ya Kadhi iliyopo kwa sasa, kama ilivyo, ina mapungufu katika kushughulikia kwa kina migogoro kuhusu ndoa za Kiislamu, kesi za talaka na masuala ya urithi

Sheikh Abubakar Bini wakati wa ufunguzi Rasmi wa Masjid Hudaa Eldoret

Viongozi wa Kiislamu katika Kaunti ya Uasin Gishu, wakiongozwa na Sheikh Abubakar Bini, wameomba serikali kuunda Mahakama ya Rufaa ya Kadhi.

VIDEO:https://vm.tiktok.com/ZMMYRKG8S/

Hii inafuatia wasiwasi uliotolewa na Sheikh Bini na viongozi wengine wa dini ya Kiislamu akiwemo sheikh Albeit  Ali kuhusu uwezo mdogo wa mfumo wa sasa wa Mahakama ya Kadhi kushughulikia migogoro inayohusiana na ndoa za Kiislamu, talaka na namna ya kugawa urithi.

“Mahakama ya Kadhi iliyopo kwa sasa, kama ilivyo, ina mapungufu katika kushughulikia kwa kina migogoro kuhusu ndoa za Kiislamu, kesi za talaka na masuala ya urithi,” walisema viongozi wa Kiislamu.

Iwapo mlalamishi hakuridhika na  uamuzi wa  mahakama ya kadhi kama ilivyo sasa hakuna namna muislamu  anaweza kukataa rufaa  uamuzi wa mahakama  hiyo na hivyo kuendelea kuwanyima haki mamia ya waislamu kwenye makahama zetu,Alisisitiza Sheikh Bini.

Kauli hizi zilitolewa wakati wa ufunguzi rasmi wa Masjid Hudaa, msikiti uliopo eneo la Sogomo na ulijengwa hasa kuhudumia mahitaji ya kidini ya  umma wa kiislamu na  haswa wanafunzi wa Kiislamu kutoka Chuo Kikuu cha Eldoret.

Sherehe ya ufunguzi ilitoa jukwaa kwa viongozi wa Kiislamu kuzungumzia wasiwasi wao kuhusu uwezo wa mfumo wa sasa wa Mahakama ya Kadhi, huku pia wakisisitiza umuhimu wa kukidhi mahitaji ya kidini ya jumuiya ya wanafunzi wa Kiislamu wa chuo kikuu cha Eldoret.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *