Ramadhan:Waislamu wa Uasin Gishu Wapokea Msaada wa Chakula kutoka kwa Serikali

0

Mamia ya Waislamu wasiojiweza katika kaunti ya Uasin Gishu watafaidika kutokana na magunia 100 ya mchele yaliyotolewa na serikali kama msaada, pamoja na magunia 400 ya maharagwe, mafuta ya kupikia, na unga

Sheikh Abubakar Bini, Naibu Mkurugenzi wa Baraza la Fatwa, anapokea msaada wa chakula kutoka kwa serikali kuwasaidia waumini wa Kiislamu wasiojiweza katika kaunti ya Uasin Gishu wakati wa mfungo wa Ramadhani.

Waislamu katika kaunti ya Uasin Gishu wamepokea msaada wa chakula kutoka kwa serikali kuwasaidia mamia ya waumini wasiojiweza ambao wanaingia katika mfungo wa Ramadhani, nguzo ya nne muhimu katika dini ya Kiislamu.

Sheikh Abubakar Bini, Naibu Mkurugenzi wa Baraza la Fatwa, amepongeza serikali ya Rais William Ruto kwa kuondoa kwa wakati ushuru wa uagizaji wa tende ambazo hutumiwa kwa wingi wakati wa mfungo wa Ramadhani.

“Tunapongeza serikali ya Rais William Ruto kwa kuwakumbuka Waislamu kwa njia ya kuwapa vyakula wale wasiojiweza na hata kuondoa ushuru wa tende,” alisema Sheikh Bini.

Waislamu kote duniani wameingia katika mfungo wa 1,435 wa Ramadhani mwaka huu wakiombea amani duniani kutokana na vita vinavyoendelea katika mataifa ya Israel na Palestina na hata Urusi na Ukraine.

Mamia ya Waislamu wasiojiweza katika kaunti ya Uasin Gishu watafaidika kutokana na magunia 100 ya mchele yaliyotolewa na serikali kama msaada, pamoja na magunia 400 ya maharagwe, mafuta ya kupikia, na unga.

Viongozi wa Kiislamu wametoa wito kwa Wakenya kuwasaidia watu wasiojiweza msimu huu wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Msaada huu unakuja wakati mwafaka kwa Waislamu wengi ambao wanakabiliwa na changamoto za kiuchumi kutokana na  kupanda kwa bei ya vyakula.

Msaada huu unaonyesha dhamira ya serikali ya kuwasaidia Waislamu na kuhakikisha wanaweza kufunga Ramadhani kwa amani na utulivu.

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *