MAMBO KUMI (10) YAKUZINGATIA UNAPOJITETEA MAHAKAMANI

0

Mambo Kumi ya kuzingatia unapojitetea mahakamani/Image Courtesy

1: Kama unahojiwa na Wakili Mahakamani usijibu bila kutafakari alichokuuliza

 

2: Wakili asikuogopeshe kwa ukali, anapokuuliza kwa ukali hulenga kuleta paniki na kukusahaulisha ulichopanga kusema

 

3: Usilazimishe kujibu kitu ambacho hukijui ni bora kusema sijui kuliko kulazimisha kujibu

 

4: Usipaniki kiasi cha kutoa neno lolote la kashfa, kejeli, au tusi mahakamani unaweza kuongeza kosa la kuidharau Mahakama

 

5: Kama hukuelewa vizuri kosa ulilosomewa ni bora kukaa kimya, kwa kuwa ukikaa kimya unaandikiwa umekataa kosa

 

6: Kanuni ya sheria ni kuwa, ni kazi ya aliyekushitaki kuthibitisha kwa ushahidi kuwa umetenda kosa na si kazi yako kuthibitisha kuwa haujatenda kosa

 

7: Kama ulitenda kosa katika harakati za kujitetea usidhuriwe iambie mahakama kuwa ulitenda kosa ukijilinda (self defence) inaruhusiwa, hata kama uliua waweza kuachiwa

 

8: Kama ndugu yako hana akili timamu na ametenda kosa iambie mahakama. Hii ni kwa sababu kutokuwa na utimamu wa akili ni kinga inabidi aachiwe lakini hatarudi nyumbani atapelekwa vituo vya walio na matatizo ya kiakili.

 

9: Inakubalika na ukaachiwa huru kusema kuwa sikuwa eneo la tukio wakati likitokea kama kweli haukuwapo

 

10: Kama wanaokushtaki wanashahidi na unamjua kuwa kuna kipindi aliwahi kuchanganyikiwa au kufanya tukio lolote la uhalifu kabla, ni nafasi nzuri kuhoji uwezo na uadilifu wake.

Courtesy

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *