Baraza la Waislamu Fatwa lapongeza uteuzi wa Kadhi mkuu Kenya !

0

-Kadhi mkuu Athman alihitimu chuo kikuu cha Azhar nchini Misri

Baraza la Waislamu la Fatwa limepongeza uteuzi wa  sheikh Abdulhalim Hussein Athman kama Kadhi mkuu Kenya .
Kupitia mkurugenzi wa baraza hili Sharif Ahmad Badawi na Naibu wake Sheikh Abubakar Bini ,wameelezea matumaini kuwa kadhi mkuu ataunganisha umma wa kiislamu Kenya.
“Tunapongeza jaji mkuu Martha Koome na tume ya huduma za mahakama JSC kutokana na uteuzi wao wa busara kumchangua Sheikh Abdulhalim Athman kuwa kadhi mkuu Kenya ,ana vigezo hitajika na hekima fika kutekeleza  jukumu Hilo la kikatiba “Sharif  Badawi
Kwa upende wake Sheikh Abubakar Bini ameelezea imani kuwa kadhi mkuu mpya ataweza kuwaunganisha  waislamu wote kama walivyofanya watangulizi wake .
Sheikh Abdulhalim ni  miongoni mwa watahiniwa watano  wanasheria waloteuliwa kupigwa Msasa na tume ya huduma za mahakama JSC .Wadhifa huo ulivutia zaidi ya wakenya 24 waliotuma maombi yao kwa tume hiyo .
Kadhi mkuu  Athman alihitimu  chuo kikuu cha Azhar nchini Misri na kisha akahudumu kama  mwalimu wa  Madrasatul Munawar Mombasa, kisha akawa Kadhi wa Kwale, Mombasa na Isiolo ,Aidha  amekuwa akishikilia wadhifa wa kinara wa kadhi mkuu kabla ya kuteuliwa kwake kuhudumu Rasmi kama kadhi mkuu Kenya .
Sheikh Athman  ametambulika kwa sifa ya ukarimu, uaminifu na uwazi katika utenda kazi, masheikh wengi wamemkubali kama mwanasheria mkweli na mcha Mungu
Sheikh Athman aliyepata elimu ya Dini kutoka kwa mashekhe mbali mbali akiwemo babake Ustadh Hussein Athman  Ni  mkaazi wa Malindi – Kilifi county , asili yake ikiwa  Kizingitini kaunti ya Lamu .

About Author

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *